Masaa kadhaa baada ya klabu ya Manchester United kukamilisha usajili
wa beki wa kimataifa wa Italia Matteo Darmian na kiungo Bastian
Schweinsteiger kutoka Bayern Munich, leo hii klabu hiyo imetangaza
kuafikiana makubaliano na Southampton juu ya usajili wa kiungo Morgan
Schnederlin.
Man United na Southampton wamekuwa na mazungumzo kwa muda wa wiki kadhaa sasa na hatimaye vilabu hivyo usiku wa kuamkia leo vilikubaliana bei ya uhamisho ya £25m kwa ajili ya Schnederlin.
Southampton walithibitisha kuikataa ofa ya kwanza ya Man United mapema wiki iliyopita, lakini yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya United kwenda kwenye Tour, hatimaye klabu hiyo imekubali ofa ya United.

Note: Only a member of this blog may post a comment.