Saturday, July 11, 2015

Anonymous

AJALI: Watu Wawili Wafariki Dunia Baada ya Gari Kupata Ajali Katika Hifadhi ya Mikumi.

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine wawili wamejeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya Toyota Hiace ilikuwa ikisafirisha magazeti ya kampuni mbalimbali kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Mbeya kupata ajali mbaya katika hifadhi ya mikumi barabara ya Morogoro Iringa.

ITV imeshuhudia gari hilo likiwa limeharibika vibaya katikati ya hifadhi ya mikumi huku likiwa limesheheli magazeti ya kampuni mbalimbali ambayo yalikua yakisafirishwa kwenda mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa mganga wa zamu katika hospitali ya St. Kizito Mikumi Dr.Hakimu Msyokege amekiri hospitali hiyo kupokea maiti mbili akiwemo dereva wa gari hilo Michael Maliwa pamoja na mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika ambapo amajeruhi wawili bado hali zao ni mbaya na wanaendelea na matibabu.

Nao ndugu wa marehemu na majeruhi wakizungumzia tukio hilo wameeleza walivyopata taarifa za ajali ambapo wamesema hawajui chanzo cha ajali hiyo.
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limethibitisha kutokea kw atukio hilo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.