Sunday, June 21, 2015

Anonymous

UREMBO HUU JAMANI! Wajua Tattoo inaweza kuzuia usinyonyeshe mtoto? Nina hii story toka Australia

Michoro ya mwilini aka tattoo ni urembo mwingine kwa watu wengi hasa vijana… Mama mmoja Australia ana mtoto mchanga lakini hatoweza kumnyonyesha mtoto wake kutokana na agizo la Mahakama !!

Vipimo vya Hospitali havijaonesha kama mama huyo ana tatizo lolote, ila ishu ni tattoo ambayo alijichora, Mahakama ilipokea malalamiko kutoka wa mume wa mwanamke huyo kuhusu tattoo aliyojichora kwenye kidole na mguuni.. wakamzuia asimnyonyeshe tena mtoto huyo kutokana na kanuni zilizowekwa na Australian Breastfeeding Association.

Bado kuna mvutano kwenye ishu ya uamuzi huo, CEO wa Australian Breastfeeding Association, Rebecca Naylor yeye anapingana na uamuzi huo wa Mahakama.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.