Mkaguzi wa Vyakula na Dawa toka Mamlaka ya TFDA, John Mosha
amesema watu wanaotumia dawa mbalimbali kuongeza na kupunguza ukubwa wa
maumbile yao wako katika hatari ya kupata saratani ya ngozi kutokana na
dawa wanazotumia kuaminika kuwa zina viambata vya sumu.
Baadhi ya dawa zilizopigwa marufuku ni pamoja na hip up cream, breast cream, lift up na fem tight.
Mosha amesema dawa hizo zina viambata sumu ambavyo vinaingia kwenye ngozi na kusababisha saratani ya ngozi.


Note: Only a member of this blog may post a comment.