Thursday, June 4, 2015

Anonymous

MVULANA AJIGEUZA MSICHANA NA KUFANYA KAZI YA U-HOUSEGIRL NA KUZUA BALAA BAADA YA KUGUNDULIKA!

Shani ramadhani
HILI na liwe onyo kali kwa familia zote Bongo. Kijana mmoja nchini Uganda aliyejulikana kwa jina moja la Daudi amebainika alijigeuza msichana kimwonekano ili apate kazi ya ndani.

Tukio hilo lilitokea nchini humo hivi karibuni ikidaiwa kuwa, mwajiri wake alihangaika sana kupata msaidizi wa kazi za ndani.Ilidaiwa kuwa, bosi wake alimpata mvulana huyo aliyejifanya msichana na kuanza kuishi naye kwa miezi nane tangu mwaka jana Oktoba bila kujua kuwa ni mvulana.

“Awali wakati anampata, mama huyo mwenye watoto wanne, wawili wakiwa wa kike alijua msaidizi wake ni msichana kama wengine, ila alijaliwa sura ya kiume ndiyo maana alionekana kama mwanaume,” kilisema chanzo.Habari zinadai kuwa, bomu lililipuka baada ya siku moja bosi wake kuibiwa fedha ndani na kumtuhumu ‘hausigeli’ huyo kwamba atakuwa anajua kwa vile ndiye anayeshinda nyumbani.

“Alimpeleka kituo cha polisi. Alipokaguliwa na polisi wa kike, wakashtuka kumwona ana matiti feki kwa kuweka nguo na kuyavalia sidiria,” kilisema chanzo.Habari hii baada ya kuonekana kwenye mitandao ya kijamii, imeleta balaa kwa wadada wa kazi wanaosaka ajira hasa katika Jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya familia, waajiri wameanza kuwakagua wasichana wanaowapata kufanya kazi za ndani wakihofia kuwa na hausigeli ambaye ni hausiboi na kulala chumba cha watoto wa kike!

Mama Severen, mkazi wa Namanga, Dar alipozungumza na Amani alisema: “Licha ya kwamba msichana wangu wa kazi ana mwaka mmoja sasa lakini nilipopata habari za yule wa Uganda niliamua kwenda kumkagua wa kwangu. Unajua ni mbaya maana hata ukaguzi wenyewe ni kama kudhalilisha.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.