Brighton Masalu
Miezi miwili iliyopita kuliibuka
madai mazito kwamba staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo mashabiki wake wakapiga
vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa tumbo hilo limeyeyuka na
yupo ‘flati skriini’.
“Hakuwa akija chuoni kwa muda, baadaye akawa anahudhuria kwa ‘kupibu’ kisha kuacha tena ila ameanza juzi tu kutokana na kuwepo kwa mitihani,” alisema mmoja wa wanachuo hao.Kama taaluma inavyoelekeza, mwandishi wetu alimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi huku ikiita bila majibu.
Baadaye alitumiwa ujumbe wa kwanza uliosomeka: “Tafadhali naomba upokee simu, nahitaji kuzungumza na wewe jambo muhimu.” Hata hivyo, hakujibu.Baada ya kuona kimya, mwandishi wetu alimtumia ujumbe ulioonesha madai hayo: “Kuna tetesi kuwa ulinasa mimba na kuficha na sasa inadaiwa kutoka na kwamba hata chuoni haukuwa ukihudhuria, hili likoje?”
Baada ya kimya cha saa kadhaa, Lulu alijibu:
“Hao wanaodai nina mimba walinipa wao? Sina nafasi ya kufafanua.”
Hivi karibuni Lulu aliripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa huenda ana mimba.

Note: Only a member of this blog may post a comment.