Wednesday, June 17, 2015

Anonymous

KIMENUKA! SIMBA SC Yampeleka MESSI Kamati ya Nidhamu

Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’.
Khadija Mngwai, Dar es Salaam
UONGOZI wa Klabu ya Simba umepanga kumfikisha katika kamati ya nidhamu ya klabu hiyo mchezaji wake Ramadhani Singano ‘Messi’ kufuatia madai kuwa mkataba wake umefojiwa.

Simba wamesema TFF wanatakiwa kuutangazia umma kuwa mkataba waliokuwa nao wao ndiyo sahihi na ule wa Messi ni feki.Simba na Messi waliingia kwenye mvutano mkubwa baada ya Messi kusema kuwa mkataba wake umemalizika wakati Simba wenyewe wana mkataba ambao unamalizika mwakani lakini TFF waliingilia kati na kuwapatanisha.

Kikizungumza na Championi Jumatano, chanzo cha habari kutoka Simba kimeeleza kuwa, Simba inatarajia kumfikisha Messi mbele ya kamati ya nidhamu ya klabu hiyo ili kujieleza juu ya kuidhalilisha klabu ikiwa ni pamoja na kuitaka TFF kutangaza hadharani kuwa mkataba wa mchezaji huyo haukuwa halali.

“Simba inaitaka TFF kuweka wazi kuwa mkataba wa Messi haukuwa sahihi ili kuondoa utata kwa kuwa mchezaji ameidhalilisha klabu kutokana na kitendo kilichotokea, pia afikishwe katika Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji ili kuchukuliwa hatua.

“Baada ya TFF kuweka wazi uongozi umepanga kumchukulia hatua mara baada ya kufikishwa katika kamati ya nidhamu ya Simba ili kutoa maelezo juu ya kile kilichotokea,” kilisema chanzo hicho.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.