“Nchi za Africa huwa tunabaki kulialia sana lakini lazima uangalie wenzako Duniani kuna nini… Changamoto ya kwanza ni Katiba.. pili ni rasilimali watu, changamoto nyingine ni tofauti zilizopo kati ya watu. Kuna tatizo la umaskini, lazima pia tuwafanye Watanzania wajitambue.. Kwenye sekta ya elimu hali ya Watanzania kufikiri iko chini sana”>>> James Mbatia.
James Mbatia, Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi
“Katika changamoto tulizonazo iko ya mama na wajawazito, katika kila watoto 100 chini ya miaka mitano, watoto 42 wana tatizo la udumavu. Changamoto ya pili ni ukosefu wa ajira na tumeanza kuona matukio kama ya panya road, watu wamepoteza matumaini kuishi kama binadamu wa karne ya 21.
Tatizo kubwa tulilonalo ni rushwa na ufisadi, lazima tuwaweke wala rushwa wote Segerea na sio kuchukua fomu za kugombea Urais”>>> Ibrahim Lipumba.
Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha CUF
“Ili nchi iwe sawa lazima mzawa wa Tanzania apewe nafasi ya kwanza. Changamoto nyingine ni ardhi, ardhi yetu nyingi inachukuliwa na wageni… Kingine ni Uchumi wan chi hii umedorora, ukiona fedha inapungua thamani hii ni dalili kwamba Uchumi unadorora. Changamoto nyingine ni afya, afya ya Watanzania ni mbovu. Changamoto nyingine ni elimu, hata ukienda kwenye midahalo na nchi nyingine utaona Mtanzania anapwaya” >>> Emanuel Makaidi.
Emanuel Makaidi, Mwenyekiti wa Chama cha NLD
“Changamoto ya kwanza tuna Uchumi usiozalisha ajira, pili tuna huduma duni za kijamii ikiwemo elimu, afya na maji… Changamoto ya tatu ni rushwa na ufisadi, changamoto ya nne ni nyufa katika nchi yetu, nyufa za udini na ukabila.. Yote haya tutayatatua kwa kuweka miiko ya Viongozi, huwezi kuwa Waziri wa Kilimo na wewe ndio una zabuni ya kusambaza Mbolea, au Waziri wa Maliasili na wewe ndio una vitalu vya kuwinda” >>> Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo
Majibu yao yako kwenye hizi sauti hapa, ukipla utawasikia wote.

Note: Only a member of this blog may post a comment.