JACQUELINE WOLPER: MIMI NI FREEMASON KWA MUDA MREFU SASA!
Staa wa bongo movie Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’.
UPO? Mtoto mzuri katika tasnia ya uigizaji Bongo,
Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’ amesema haoni sababu ya
kuukana uanachama wa taasisi ya Wajenzi Huru (Freemason) kwani ni dini
kama zilivyo zingine na kama katiba inavyoelekeza, kila mtu anayo haki
ya kujiunga na dini au taasisi yoyote ya kuabudu kulingana na matakwa ya
imani yake.
Jacqueline Wolper Massawe akiwa katika pozi.
Akichezesha taya na Amani, Wolper alisema ni kweli
yuko katika kundi hilo huku akishangaa watu kustaajabu kuona mtu yuko
Freemason wakati walioanzisha dini hiyo ni binadamu kama wengine.
“Freemason si ni taasisi au dini kama zingine? Kuna ajabu gani mimi
kuwa mwanachama? Tena nataka nikuhahakikishie kuwa, nimekuwa muumini
halisi wa Freemason kwa muda mrefu sasa,” alisema Wolper.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
WASANII
on Thursday, June 25, 2015
Note: Only a member of this blog may post a comment.