Na Makongoro Oging’
“Nisaidieni mwanangu awe kama watoto wengine,” ni maneno ya mama
mzazi wa mtoto Azimina Abdallah (miezi 11), mkazi wa Zanzibar, Unguja
anayeishi kwa mateso na maumivu makali kutokana na jicho kuvimba tangu
azaliwe.
Kwa
sasa mama mzazi wa mtoto huyo aitwaye Amina Mbaruku anahangaika naye
huku baba yake akidaiwa kutoonekani kwa muda mrefu, hivyo kuchukua
uamuzi wa kuiomba jamii imsaidie.
MAUMIVU MAKALI APATAYO MTOTO
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita katika Hospitali ya
Muhimbili, Taasisi ya Mifupa na Mishipa (MOI), Wodi A ya Watoto, mama
huyo alisema kwamba maumivu anayoyapata mwanaye siyo ya kawaida na hata
yeye hapati usingizi kutokana na mtoto wake kulia usiku kucha.
KUZALIWA KWAKE
Mama huyo aliendelea kusema:
“Mwanangu nilijifungua katika zahanati iliyopo Kijiji cha Kivunje,
Unguja akiwa na tatizo hili la uvimbe na kila anapokua na uvimbe pia
unakua huku ukimsababishia maumivu makali. Tulihamishiwa Hospitali ya
Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya hali yake kuwa mbaya.
KIPIMO CHA SH 450,000
“Mwezi wa tatu mwaka huu tulikuja Muhimbili kwa matibabu zaidi,
baadhi ya vipimo vilifanyika lakini kuna kipimo kinahitajika kifanyike
katika hospitali binafsi ambacho gharama yake ni shilingi laki nne na
nusu fedha ambazo sina.
“Mume wangu anayefanya shughuli ya kuuza nazi alinikataza nisije
Muhimbili kwa sababu hana uwezo wa kutusafirisha pia alidai hana fedha
ya kunitumia kwa ajili matumizi, alinishauri nibakie kule nyumbani ili
tuwe tunatumia miti shamba, sikukubali.
“Niliwaona madaktari wa Zanzibar, nilipowaeleza kwamba mume wangu
hakuwa na uwezo walinisafirisha mimi na mwanangu hadi hapa Muhimbili.
“Nashukuru tumefika lakini napata shida sana hata fedha za vipimo na za kumnunulia mtoto pampasi sina.
“Nawashukuru madaktari na wauguzi wa hapa MOI wanavyonisaidia kadiri
ya uwezo wao, lakini kuna huduma zingine ambazo hazipatikani hapa kama
ya kipimo cha T Scan.
“Watoto wangu wengine watatu nimewaacha na mama wa kambo
anayejishughulisha na kilimo cha mihogo, hata hivyo bado wana matatizo
makubwa sana, baba yao tangu nimefika hapa hajawahi kunipigia simu na
nimesikia ameondoka nyumbani.
Napenda kuwasiliana naye ili nimweleze kinachoendelea lakini nashindwa.
“Napata shida sana na huyu mtoto lakini nitahakikisha napambana hadi
hatua ya mwisho, siwezi kumuacha kwani nampenda sana, ninachoomba kwenu
Watanzania wenzangu mnisaidie ili mwanangu apone aweze kufurahia maisha
kama watoto wengine wenye afya njema,” alisema mama huyo.
Kwa yeyote ambaye yupo tayari kumsaidia mtoto huyo awasiliane na
mama yake au amsaidie kwa kupitia simu ya muuguzi wake Muhimbili kwa
namba 0719 626520 au 0783 536320.
Tuesday, June 23, 2015
HUJAFA HUJAUMBIKA! MATESO ANAYOPATA MTOTO HUYU USIOMBE YAKUKUTE!
JE, UMEZISOMA HABARI HIZI?

Rais Magufuli Asema Bei ya Umeme HAITAPANDA Hata Kidogo... Ampongeza Waziri Muho...

POLE POLE Asema CCM Inahitaji Viongozi Waliojikita Katika Imani ya Chama!

ZITTO Kabwe: Mwaka 2016 Ulikuwa wa Utumbuaji Majipu na Kusahau Kuboresha Maisha ...

Cheki Hapa Matokeo ya Mtihani wa Darasa la nne 2016 na Form Two 2016

Matokeo ya Kidato cha Pili Yatangazwa... Yacheki Hapa! Pia Tazama Top 10 za Mwan...

‘Nilikwepa Mawe Manne Kabla ya Kuchomwa Mkuki Mdomoni’ - Augustine Mtitu
Note: Only a member of this blog may post a comment.