GLADNESS MALLYA
DOKTA Chale ambaye anaandika makala za afya katika
gazeti ndugu la hili la Ijumaa, ameanika chanzo cha mastaa wengi kupata
ugumba ambapo pamoja na vyanzo vingine, ameyataja madawa ya kuongeza
maumbile ya mwili na ya kujichubua yanasababisha tatizo hilo.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumzia madawa hayo pasipo kuyataja majina (yamezagaa mitaani),
dokta Chale alisema baadhi ya madawa hayo yana kemikali ambazo hupenya
hadi kwenye figo na kuzisababishia madhara ambapo moja kwa moja hawezi
tena kupata mtoto. Alisema amekuwa akisikia kila kukicha katika vyombo vya habari mastaa wakijieleza kuwa wamehangaika sana kupata watoto lakini imeshindikana pasipo kujua madawa hayo ndiyo chanzo hivyo ni vyema wakachukua tahadhari.
“Kwa wale ambao bado hawafikirii kuzaa ni vyema wakawa makini na madawa haya ya kuongeza maumbo yao. Yanaathiri figo na zikishaathirika mwanamke hawezi tena kupata ujauzito.
Miongoni mwa mastaa ambao wamesharipotiwa kuwa na tatizo la kukosa watoto kwa muda mrefu ni pamoja na mbunge mtarajiwa, Wema Sepetu ‘Madam,’ Judith Wambura ‘Jide,’ Rehema Chalamila ‘Ray C’ (pichani), Mainda Suka, Jacqueline Wolper na Jokate Mwegelo ‘Kidoti.’

Note: Only a member of this blog may post a comment.