Sunday, June 21, 2015

Anonymous

Baada ya Kushambuliwa kwa Kumpa Break Nuh Mziwanda, SHILOLE KIUNO Ajibu Mapigo!

Baada ya Shilole kutangaza kumpa break mwenzi wake Nuh Mziwanda kwa muda wa mwezi huu mzima, wakitarajia kuendeleza malavi davi yao baada ya kipindi hiki kitakatifu kupita, baadhi ya mashabiki ambao wanajinasibu kuijua dini wamekuwa wakimshambulia Shilole kwa maneno kwenye mitandao ya kijamii kuwa kitendo cha kutaka kumrudia tena Miziwanda bila ndoa sio sawa kwa upande wa dini na wengine kwenda mabli zaidi na kudai hata kazi yake ya sanaa ambayo humfanya kukata maouno pia haifai, kitendo ambacho kimepelekea Shilole kujibu mapigo kwa kuandika jina lake kamili na kusema ni Mungu pekee ndio anamjua na sio binadamu.

“Zuwena Mohamed bint Yusuph anaeyenijua ni Mungu pekee na si binaadam” –Shilole ambaye jina lake ni Zuwena Mohammed alindika hayo mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu.

Jamani tuacheni kuwanyooshea kidole watu wakati vingiune vinakusonta wewe.
Mzee wa Ubuyu

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.