Aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid.
Imelda mtema ALIYEKUWA mshiriki
wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid hivi karibuni amedaiwa kufukuzwa
kwenye msiba mmoja maeneo ya Mbezi mara baada ya kuonekana akijipiga
picha (selfie) na kujichukua video akiwa ghorofani. Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku ya tukio, Husna akiwa msibani hapo, kwa sababu anazozijua mwenyewe, alipanda ghorofani kwenye nyumba hiyo yenye msiba na kuanza kujipiga picha hizo kitendo ambacho kilionekana kuwakera wafiwa.
“Alipanda ghorofani akaanza kufanya mambo hayo ya kujipiga picha utadhani tupo kwenye sherehe,” kilisema chanzo hicho na kuendelea:Mara baada ya tukio hilo la ajabu, wafiwa wakaamua kumfuata Husna kulekule ghorofani na kumwambia ashuke na aondoke zake, akaondoka. Husna alipopigiwa simu, alijibu: “Siyo kweli, wananichafua tu.”


Note: Only a member of this blog may post a comment.