Ijumaa: Mara nyingi umekuwa siyo mtu wa kutulia nchini kwani muda mwingi unakuwa Nairobi, nini siri ya safari zako?
Sabby: Unajua robo tatu ya maisha yangu ni Nairobi kwani nimekulia huko na nimefanya vitu vingi nikiwa huko, ndiyo maana mara nyingi nakuwa huko.
Ijumaa: Wewe ni msichana mrembo sana je, ni changamoto gani ulizokutana nazo ulipoingia katika tasnia ya filamu?
Sabby: Changamoto kubwa ni baadhi ya wanaume kutaka kunitumia kama Big G.
Ijumaa: Vipi kuhusu uhusiano wenu wa kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Bob Junior uliishia wapi?
Sabby: Nafikiri kila mmoja hakuwa na malengo thabiti na mwenzake hivyo tuliamua kila mmoja achukue hamsini zake.
Ijumaa: Je, ni mwanaume gani sahihi unayemhitaji katika maisha yako?
Sabby: Mwenye kujali na kunithamini, kuhusu pesa ni kitu cha mwisho kabisa katika mapenzi.
Ijumaa: Siku hizi mastaa wengi hawajali kuolewa bali wanatafuta mtu na kuzaa naye, vipi kwa upande wako?
Sabby: Mimi nina mtoto tayari wa kiume, nampenda sana na kwa sasa ana umri wa miaka minne.
Ijumaa: Ukimpata mume wa maisha yako, unahisi ni kitu gani utakifanya?
Sabby: Ukweli najivunia kwamba najua kupika kila aina ya chakula na ninaamini mwanaume yeyote anapenda kupikiwa vizuri, mimi uchawi wangu pamoja na mambo mengine utakuwa kwenye mapishi.
Ijumaa: Ulishawahi kuwa na uhusiano na staa yeyote wa kiume wa Bongo Movies?
Sabby: (Ndiyo), lakini sipendi kumtaja jina na tuliachana muda mrefu sana.
Ijumaa: Unafikiri kama atajitokeza msanii kutoka Bongo Movies akataka kukuoa itakuaje?
Sabby: Sitaki kabisa maana siwezi tabia zao ni ngumu sana na hatuwezi kudumu kwa sababu kuna usemi usemao mafahari wawili hawaishi zizi moja.
Ijumaa: Je, ulishawahi kushawishiwa kucheza filamu za utupu?
Sabby: Kuna jamaa mmoja alishanieleza jambo hilo nikiwa Marekani lakini nilimwambia mila na desturi zetu hazikubali vitu hivyo.
Ijumaa: Mara nyingi mastaa wa Bongo Movies mnalalamikiwa kuiba waume za watu, unazungumziaje hilo?
Sabby: Ni kweli tabia hizo zipo na hiyo inatokana na mastaa wengi hatuolewi hivyo inawabidi wabanane hapohapo.


Note: Only a member of this blog may post a comment.