Friday, May 15, 2015

Anonymous

MAKUBWA NA MAZITO HAYA: MAIMARTHA AMUUMBUA MDADA SAJENT WA BONGO MUVI!

Na Hamida Hassan
Kumekuwa na madai kuwa, mwanadada Husna Sajent ameolewa na msanii mwenzake wa filamu, Salim Ahmed ‘Gabo’ lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha! Hata hivyo, juzikati Maimartha Jesse ‘Mai’ alimwaga mchele mbele ya kuku kwa kumuita Husna ‘Mrs Gabo’.

Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mai alifanya hivyo pale alipokuwa akiwatambulisha mastaa waliohudhuria sherehe ya ‘baby shower’ ya Aunt Ezekiel iliyofanyika Mwendopolepole, Bagamoyo mkoani Pwani.
Katika utambulisho huo, Mai alimuita Husna ‘Mrs Gabo’ akimaanisha na si kwa utani, hali iliyowafanya watu kuanza kunong’ona kwa chini na kumuacha Husna akicheka asijue namna ya kuua soo.
Msanii wa filamu za Kibongo, Husna Sajent.
“Si mwenyewe anasema ile picha iliyovuja akionekana kafunga ndoa na Gabo ni filamu, sasa kumbe watu wake wa karibu wanajua ukweli, mh! Makubwa,” alisikika akisema dada mmoja aliyekuwa eneo hilo la sherehe.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.