Na Musa Mateja
ILIANZA kama utani lakini siku zilivyosonga ndivyo uhusiano wao ulivyowekwa wazi, hao ni watu wawili waliowahi kuwa maadui wakubwa miaka kadhaa nyuma.
Staa wa filamu Shamsa Ford na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ wakifanya yao.
Hapo nawazungumzia staa wa filamu Shamsa Ford na msanii wa Bongo
Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambao kwa sasa wamezama kwenye
mahaba niue.
Awali, wahusika wote walitumia nguvu kubwa kukanusha juu ya uhusiano wao lakini inatajwa kuwa mahaba yao ndiyo gumzo kuliko ya wengine wote katika Bongo Muvi na yanashika nafasi ya pili katika Bongo Fleva nyuma ya Diamond na Zari kwa sasa.
Awali,
uadui wao ulitokana na Nay kuwaponda wasanii wa kike wa Bongo Muvi na
kudai wengi wao hawana lolote na kazi yao ni kujiuza, Shamsa alikuwa
mmoja wa waliopokea kwa hasira kali na kumbwatukia Nay lakini ule usemi
kuwa ‘wagombano ndiyo wapatanao’, ulikuwa unawahusu.
Walipoulizwa
juu ya mahabati yao baada ya picha kuvunja mitandaoni wakipeana
‘mabusu’ motomoto hivi karibuni, walisema wana ‘project’ maalum ya
filamu.
Sasa inavyoonekana filamu yao imekuwa ya ukweli badala ya zile za kuigiza. Pichani ni jinsi mahaba nigaragaze yalivyotawala katika maisha ya wawili hao.

ILIANZA kama utani lakini siku zilivyosonga ndivyo uhusiano wao ulivyowekwa wazi, hao ni watu wawili waliowahi kuwa maadui wakubwa miaka kadhaa nyuma.
Awali, wahusika wote walitumia nguvu kubwa kukanusha juu ya uhusiano wao lakini inatajwa kuwa mahaba yao ndiyo gumzo kuliko ya wengine wote katika Bongo Muvi na yanashika nafasi ya pili katika Bongo Fleva nyuma ya Diamond na Zari kwa sasa.
Sasa inavyoonekana filamu yao imekuwa ya ukweli badala ya zile za kuigiza. Pichani ni jinsi mahaba nigaragaze yalivyotawala katika maisha ya wawili hao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.