May 26 2015 siasa zimeendelea kutawala kwenye Headlines kwenye kurasa za Magazeti TZ.
Iko stori ya Baraza la Madiwani Manispaa
ya Kinondoni limependekeza kuongezeka kwa Majimbo ya Uchaguzi Wilaya ya
Kinondoni, Rais JK
amemteua Mkuu mpya wa Wilaya na wengine 10 kuwabadilisha vituo vyao vya
kazi.. nyingine inahusu Rais JK kuwaonya vijana wa CCM walio vyuoni
kuacha kutumiwa kama makuwadi.
Askari wawili Rukwa wanashikiliwa kutokana na upotevu wa SMG kwenye kituo cha Polisi, Mzee Cleopa Msuya
amesema TZ inahitaji Rais dikteta.. stori nyingine inahusu mrembo
mwenye asili ya India kugombanisha matajiri wawili Dar ambao walizidiana
dau, UKAWA wamesema wakipita kwenye Urais 2015 watapitisha Serikali ya
mseto, Waziri Membe amesema atatangaza nia yake kugombea Urais akiwa Kijijini kwao.
Kasikika pia Mbunge Edward Lowassa akizungumzia tatizo la ajira TZ na elimu, stori zote ziko kwenye hii sauti hapa kutoka #PowerBreakfast @CloudsFM.


Note: Only a member of this blog may post a comment.