Andre
Schurrle anaweza kuwa ameondoka katika ligi kuu ya Uingereza na kwenda
kucheza katika ligi ya nyumbani kwao Ujerumani tangu mwezi January mwezi
huu – lakini jambo hilo halijaweza kumfanya akose nafasi ya
kujikusanyia medali ya ubingwa wa Premier League.
Winga
huyo wa kijerumani, ambaye alihamia Wolfsburg kutoka Chelsea wakati wa
dirisha la majira ya baridi, aliichezea Chelsea mechi 14 msimu kabla ya
kuhama – hivyo kupata uhalali wa kujipatia medali ya ubingwa wa EPL.
Sheria za EPL zinaeleza ili mchezaji awe na hadhi ya kupata medali ni lazima awe ameitumikia klabu yake zaidi ya mechi 5.
Schurrle
hakuwa na ufahamu wa sheria hii, lakini wiki iliyopita kocha wa Chelsea
Jose Mourinho alimpigia simu mchezaji huyo na kumpongeza kwa
kujishindia medali ya ubingwa wa EPL baada ya Chelsea kutawazwa kuwa
mabingwa wapya wa ligi hiyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.