Tuesday, May 26, 2015

Anonymous

HAWA NDIO WAKUU WAPYA WA WILAYA WALIOTEULIWA NA RAIS KIKWETE...YUPO WAKILI MCHAPAKAZI ANTHONY PETER MAVUNDE!

  Ndugu.Anthhony Peter Mavunde-Mkuu mpya wa wilaya ya Mpwapwa
Baada ya Mkuu huyo mpya wa wilaya ya Mpwapwa ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma  Mhe.Anthony Peter Mavunde alifunguka jambo lililomfurahisha sana kwa jamii inayomzunguka akikumbuka shule yake ya msingi aliyosoma kwa kusema.....

.''Nawashukuru sana wanafunzi wenzangu wa Mazengo Primary School ambao tulishiriki pamoja kuchangia marekebisho ya vyoo na upakaji rangi wa madarasa.

Mafundi wamekamilisha awamu ya kwanza kama mnavyoona katika picha naendelea kuwaomba tujutahidi tumalizie awamu iliyobaki.

Michango yenu bado muhimu sana.Ahsanteni sana

Mtandao wa Masama Blog unampa pongezi nyingi sana mkuu mpya wa wilaya ya mpwapwa pamoja na wakuu wa wilaya wote walioteuliwa leo tukiamini mtaleta mabadiliko katika wilaya zetu na kuongeza kasi ya maendeleo ya Taifa..


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini.

Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu, 2015.

Wakuu wengine wa wilaya ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Dkt. Jasmine Tisike kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya ya Dodoma, Agnes Elias Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma kwenda Wilaya ya Tunduru, mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu kutoka Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Mkalama.

Wengine ambao wamehamishwa ni Chande Bakari Nalicho kutoka Wilaya ya Tunduru kwenda Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka Wilaya ya Mvomero kwenda Misenyi, Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Biharamulo, mkoani humo humo, Elias Choro John Tarimo kutoka Wilaya ya Biharamulo kwenda Chunya, Mkoa wa Mbeya na Deodatus Lukas Kinawiro kutoka Wilaya ya Chunya kwenda Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Mei, 2015

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.