Hii ni mara ya pili kwa nchi ya Nepal
kukumbwa na tetemeko la ardhi ambalo linadaiwa kuua zaidi ya watu 40
huku kukiwa na idadi kubwa ya majeruhi na kuacha watu wakiwa na hofu ya
maisha yao na kuishi kwa mashaka makubwa.
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo
hakuwa nyuma baada ya kuguswa na kinachoendelea nchini humo na kuamua
kutoa mchango wake kwa ajili ya kusaidia waliopatwa na maafa.
Ronaldo ametoa sehemu ya fedha zake pauni milioni 7 ilikusaidia walioathirika na tetemeko hilo la ardhi.
April 25 kulitokea tetemeko la ardhi lililoua zaidi ya watu 8000 huku maelfu ya watu wakikosa sehemu za kuishi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.