Thursday, May 14, 2015

Anonymous

AT amsifia DIAMOND Platinumz kwa uamuzi wake wa kufanya mduara!

Mfalme wa Mduara, AT, amemsifia Diamond Platnumz kwa uamuzi wake wa kufanya wimbo wa mduara ‘Nasema Nawe’ aliomshirikisha Khadija Kopa.
11189211_1117843588242633_1904760808_n
Akiongea na 255 ya XXL kwenye kipindi cha Clouds FM jana, AT alisema kuwa Diamond amefanya jambo la muhimu kufanya nyimbo za nyumbani.
“Kiukweli mimi nimefurahi kwamba amejitambua,” alisema AT.
“Unajua ukimuona msanii ambaye anafanya vizuri ametambua kwao ni wapi inabidi msherehekee nyote. Lengo kubwa hatutaki kuwa watumwa wa muziki mwingine. Tunapenda tufanye muziki wetu, watu wengine ndio watufuate.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.