HABARI za leo wapendwa wasomaji wa safu hii. Ni
tumaini langu kuwa wote mnaendelea vyema na shughuli za kila siku, hasa
katika wakati huu ambao tumetoka katika Sikukuu ya Pasaka, ambayo
ninajua wengi wenu itakuwa imewakausha mifuko yenu, maana kama siyo wewe
mwenyewe na mwenza wako, basi watoto walikaba koo kutaka mambo flani.
Juzikati, nilipata sms moja kati ya nyingi ninazopata toka kwenu wasomaji wangu na baada ya kuisoma, nikaoni ni jambo jema kama nitawashirikisha, kwa vile ninajua kabisa kuwa itatusaidia sisi kama jamii kuweza kutambua baadhi ya makosa tunayofanya katika uhusiano wetu wa kimapenzi na watu tusiowafahamu undani wao vizuri.
Mtu huyo mwanaume, aliniambia kuwa alikutana na msichana mzuri, mrembo na mwenye maisha mazuri. Alikuwa na gari zuri na hakuonekana kuwa na matatizo kama ilivyozoeleka kwa wanawake wengi. Wakaingia katika uhusiano wa kimapenzi.
Alishangazwa na ukarimu na mapenzi ya aina yake kutoka kwa huyo dada, kwani mara kadhaa alipopatwa na uchovu kiakili au kikazi, msichana alikuwa tayari kukodi chumba katika hoteli nzuri, wakaenda kupumzika huku akimpa mahaba na simulizi nzuri za kuburudisha.
Lakini siku moja, anakumbuka mdada huyo alimchukua tena na kumpeleka hoteli, akiwa huko wakila na kunywa, alijikuta akiamka asubuhi akiwa hoi, ingawa dada huyo alikuwa pembeni yake. Siku chache baadaye, alipokwenda benki, alishangaa kuona kiasi kikubwa cha fedha zake kimechukuliwa na alipofuatilia, alishangaa kuonyeshwa picha ya kijana asiyemjua, akichukua fedha kwenye akaunti yake.
“Nilimuona
ni mwanamke mwenye mapenzi ya dhati kwangu, alinipa pombe nyingi nikiwa
hotelini kumbe nikampa pasiwodi yangu ya benki bila kujijua,”
analalamika kaka huyo.Kilichopo ni kwamba wapo wanawake na wasichana
ambao wizi wa namna hiyo ndiyo maisha yao mjini. Wanaanza kukusoma,
wanajua wazi kipato chako na hata benki unakohifadhi fedha zako.
Wakishajua hivyo, ndipo wanaanza kubuni mbinu za kukuingia baada ya kuzisoma nyendo zako. Utashangaa msichana anakuagizia kinywaji katika baa yako ya kila siku, ukajiona unapendwa!Ninachotaka kuwaambia wasomaji, bila kujali kama wewe ni mkaka au mdada, ni kuwa makini na mtu unayeanzisha naye uhusiano kwa mara ya kwanza, kwa sababu katika maisha magumu kama tunayoishi, kila mtu ana malengo tusiyoyajua.
Siku zote, katika kuanzisha uhusiano mpya, lazima ujitahidi kwa kadiri unavyoweza, kujiridhisha kuwa mwenza wako ni mtu sahihi, uliyekutana naye katika mazingira muafaka na anafaa kuwa mume au mkeo mtarajiwa. Chunga sana!
Juzikati, nilipata sms moja kati ya nyingi ninazopata toka kwenu wasomaji wangu na baada ya kuisoma, nikaoni ni jambo jema kama nitawashirikisha, kwa vile ninajua kabisa kuwa itatusaidia sisi kama jamii kuweza kutambua baadhi ya makosa tunayofanya katika uhusiano wetu wa kimapenzi na watu tusiowafahamu undani wao vizuri.
Mtu huyo mwanaume, aliniambia kuwa alikutana na msichana mzuri, mrembo na mwenye maisha mazuri. Alikuwa na gari zuri na hakuonekana kuwa na matatizo kama ilivyozoeleka kwa wanawake wengi. Wakaingia katika uhusiano wa kimapenzi.
Alishangazwa na ukarimu na mapenzi ya aina yake kutoka kwa huyo dada, kwani mara kadhaa alipopatwa na uchovu kiakili au kikazi, msichana alikuwa tayari kukodi chumba katika hoteli nzuri, wakaenda kupumzika huku akimpa mahaba na simulizi nzuri za kuburudisha.
Lakini siku moja, anakumbuka mdada huyo alimchukua tena na kumpeleka hoteli, akiwa huko wakila na kunywa, alijikuta akiamka asubuhi akiwa hoi, ingawa dada huyo alikuwa pembeni yake. Siku chache baadaye, alipokwenda benki, alishangaa kuona kiasi kikubwa cha fedha zake kimechukuliwa na alipofuatilia, alishangaa kuonyeshwa picha ya kijana asiyemjua, akichukua fedha kwenye akaunti yake.
Wakishajua hivyo, ndipo wanaanza kubuni mbinu za kukuingia baada ya kuzisoma nyendo zako. Utashangaa msichana anakuagizia kinywaji katika baa yako ya kila siku, ukajiona unapendwa!Ninachotaka kuwaambia wasomaji, bila kujali kama wewe ni mkaka au mdada, ni kuwa makini na mtu unayeanzisha naye uhusiano kwa mara ya kwanza, kwa sababu katika maisha magumu kama tunayoishi, kila mtu ana malengo tusiyoyajua.
Siku zote, katika kuanzisha uhusiano mpya, lazima ujitahidi kwa kadiri unavyoweza, kujiridhisha kuwa mwenza wako ni mtu sahihi, uliyekutana naye katika mazingira muafaka na anafaa kuwa mume au mkeo mtarajiwa. Chunga sana!

Note: Only a member of this blog may post a comment.