Friday, April 24, 2015

Anonymous

VURUGU AFRIKA KUSINI: Maandamano yatikisa jiji la Johannesburg!

Raia wa kigeni wakiwa wamebeba mabango ya kupinga ubaguzi.
Hapo jana maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini waliandamana katika mji mkuu wa kibiashara wa Johannesburg kupinga mashambulizi na unyama dhidi raia wa nchi za kigeni. 
Waandamanaji hao walionekana wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa: “Sisi Sote ni Waafrika”.
Waziri Mkuu wa mkoa wa Gauteng, David Makhura, ambaye aliwahutubia waandamanaji hao alisema Waafrika Kusini watashinda chuki na mashambulizi yanayowalenga raia wa kigeni kama walivyoshinda utawala wa ubaguzi wa rangi.

Mashambulizi ya wiki kadhaa dhidi ya raia wa kigeni katika miji mikubwa ya Afrika Kusini kama Johannesburg na Durban, yamesababisha vifo vya watu wasiopungua saba

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.