Picha
za kwanza za ndege binafsi inayotoa huduma za kihoteli zaidi angani
zimetolewa na kampuni ya Canada ikiwa ni ndege inayomilikiwa na hoteli
za Four Seasons.
Ni ndege iliyopangwa kifahari ndani yake na ina uwezo wa kubeba watu
52 kwa jinsi ilivyotengenezwa ndani yake na ikawa ina nafasi kwa kila
mtu kukunjua kiti chake na kukifanya kama kitanda ambapo kama ingekua ni
ndege ya kawaida nafasi hiyo ingefikisha viti karibu 150.

Note: Only a member of this blog may post a comment.