Tuesday, April 14, 2015

Anonymous

Trafiki na dereva wa bodaboda wamepata ajali na kufariki.. kisa ni ishu ya rushwa?


random-wallpapers-candle-light-photography-wallpaper-31284
Afisa mmoja wa Polisi Kenya na dereva wa bodaboda wamefariki baada ya kupata ajali.. taarifa kutoa kituo cha K24 wamesema ishu ilianzia Afisa huyo alipomkamata jamaa mmoja na kumdai rushwa, jamaa aligoma kutoa kiasi cha pesa ambacho Afisa huyo alikitaja.

Baada ya mtu huyo kugoma kutoa rushwa ambayo Afisa huyo aliitaja, alimtoroka na kukimbia.. Askari akamsimamisha jamaa wa bodaboda ili wamkimbize, safari yao haikufika mbali.. walipata ajali hiyo kwa kugongana na gari ndogo.
Kuna mtu alikuwa amemshika akiwa amebeba begi sasa huyo mtu alimpatia elfu moja yule Askari akakataa.. alipokataa huyo jamaa akachomoka akavuka akaingia kwenye matatu iliyokuwa imetelemka hivi”–alisema mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.

Ajali hiyo ilifanya dereva wa pikipiki na Askari huyo kufariki eneo la tukio.
Kutokana na Sheria za nchi hiyo Polisi haruhusiwi kupanda gari lolote wala pikipiki anapomkamata mtu.
Nimekuwekea taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24…

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.