Friday, April 17, 2015

Anonymous

STAA WA BONGO MUVI MWENYE FIGA MATATA, AMANDA AFUNGUKA KUHUSU KASHFA YA KUTUMIA ARV

Hamida Hassan
Staa mwenye ‘figa’ matata, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni aligeuka mbogo kwa shabiki wake aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi.

Staa mwenye ‘figa’ matata, Tamrina Posh ‘Amanda’.
Ishu ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya Amanda akipima ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo alipokomenti kwamba eti msanii huyo ana ngoma.Akizungumza na Ijumaa, Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu mtandaoni wakidhani kila msanii ni mhuni.
“Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote tunatumia ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,” alisema Amanda.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.