Friday, May 1, 2015

Anonymous

SARAKASI ZA MAPENZI BONGO MUVI: KWELI Wadada wahuni walio na viwango wanapatikana Huko!

KUNA kelele nyingi katika mitandao ya kijamii na mitaani kuhusu maisha ya waigizaji na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kwa jumla.Watu wanahoji umakini wao katika mahusiano ya kimapenzi wanayoanzisha na kuyaendesha, wakiamini baadhi yao wanaigiza zaidi kuliko uhalisia wao.

Baadhi ya wakosoaji, hata hivyo, licha ya kukiri migogoro ya ndoa na uhusiano imegubika sehemu kubwa ya jamii inayotuzunguka, wanaamini tabaka la waigizaji wa filamu nchini, linashikilia nafasi ya kwanza katika kumomonyoka, kama wanavyojaribu kutoa mifano kadhaa ya uhusiano huo. 

Wema Sepetu anaongoza orodha ya waigizaji warembo ambao uhusiano wao wa kimapenzi hautoi sura ya kuvutia, hasa kutokana na msururu wa wanaume ambao wanatajwa kushiriki naye. Lakini ukiachana naye, hata wasanii wengine wenye majina makubwa, hakuna hata mmoja anayeweza kujivunia kudumu katika ndoa au uhusiano wake wa kimapenzi, kuanzia akina Kajala Masanja, Aunt Ezekiel, Johari, Chuchu Hans, Mainda, Rose Ndauka na wenzao, kuwataja kwa uchache. 

Na unaweza kudhani labda ni wanawake tu, lakini hata wanaume, nao wanaishi zaidi kwa maigizo kuliko uhalisia wao, kwani hadi hivi sasa, wapo waigizaji kadhaa ambao ndoa au uhusiano wao haujakaa vizuri, kutokana na kuhusishwa na mapenzi nje ya wenza wao wanaojulikana. 

Na mfano wa hivi karibuni zaidi, ni uhusiano kati ya waigizaji wawili, Halima Yahaya ‘Davina’ na Mike Sangu. Hawa wote wako katika ndoa, lakini bahati mbaya sana, ndoa zao ziko hatarini kuvunjika kwa sababu ya ukaribu uliopo baina yao. 

Mike Sangu ni mume wa Salome Urassa ambaye anafahamika kama Thea na Davina ni mke wa Abdallah Shakoor. Wote wanakataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi kati yao, lakini wanakiri ndoa zao kutikisika kwa sababu ya tuhuma hizo. 

Sitaki kuwahukumu kwa sababu ushahidi utanipa tabu, lakini itoshe tu kusema kuwa uzoefu unaonyesha maisha ya kimapenzi katika Bongo Movies yamejaa zaidi sanaa kiasi cha kuleta picha mbaya. Ni vigumu pia kushindwa kukubaliana na Nay wa Mitego aliyedai kuwa wadada wahuni walio na viwango wanapatikana huko. 

Kucheza kwao filamu na kuonekana, wanachukulia kama soko la kuuza sura. Umaarufu wao unawafanya waamini kuwa wao ni wazuri na wanaohitajika kuliko wanawake wengine, wakati ukweli ni kwamba wanaume wengi wakware wanaamini ni rahisi zaidi kuwapata wao kutokana na tamaa zao kuliko wanawake wanaojiheshimu. 

Ndiyo maana waigizaji wa kike wanaogopa sana maisha ya ndoa, bado akili yao inaamini mwanaume mmoja zaidi, mwenye nazo anakuja, matokeo yake umri unazidi kuwatupa mkono na wenyewe wanazidi kupitwa na wakati. Kila anayeolewa, anataka kuishi maisha ya kwenye sinema kwa mumewe, kitu ambacho kinawashinda. 

Wanataka kuleta ustaa kwenye ndoa zao. Mume akitaka kumdhibiti, anajidanganya na contacts nyingi zilizomo kwenye phonebook yake, anadhani maisha ya kila siku club ni ya kudumu. Ni bahati mbaya tu kwamba hawataki kujifunza kupitia maisha yao ya jana, leo na kesho. Laiti wangetambua kuwa wanaume wote wanaowapa jeuri hapa mjini ni waume za watu, wangeweka pembeni uigizaji.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.