Sakata la msichana wa Kitanzania, Ummul- Khayr Sadri Abdulla
ambaye amedaiwa kutaka kujiunga na kikundi cha ugaidi cha Al-Shabaab
linazidi kuchukua sura mpya baada ya madai kuwa alitoroka chuoni Sudan
wiki moja kabla ya kukamatwa Kenya.
Msichana huyo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Afrika kilichopo Sudan alikuwa akisomea udaktari mwaka wa tatu, kabla ya kukamatwa Machi 30 mwaka huu alikuwa ameshatoroka chuoni hapo tangu Machi 22 na ndugu zake walikuwa wanamtafuta.

Akizungumza na gazeti la NIPASHE babu wa msichana huyo Nassor Said Nofli, alisema kuwa taarifa za kupotea zilitolewa na dada yake mkubwa ambaye pia anasomea udaktari mwaka wa nne katika chuo hicho kitu ambacho kiliishtua familia hiyo.
Babu huyo amesema ilipofika Jumanne ilitolewa taarifa kwa baba yake aliyeko Oman kikazi, Dk. Sadri Abdulla Said pamoja na ndugu wengine waliopo Pemba, Unguja na Dar es Salaam.
“Hizi
taarifa za kupotea kwa binti yetu zilitushtua na ilitulazimu kuomba
maombi maalum ya kumuombea “Dua” ili aweze kuonekana na akiwa salama kwa
sababu Sudan kama unavyoielewa ni nchi yenye matatizo ya kivita ” alisema babu huyo.
“Kitendo
cha polisi kumkamata imetusaidia na pia wamesaidia kumuokoa yule mtoto
kutokujiingiza kwenye hicho kikundi kwani angeweza kuuliwa ama kupotea
katika kundi hilo,”– Nofli.
Alieleza kuwa mbali na binti wao kuendelea kushikiliwa na polisi, wanaamini kuwa vyombo vya sheria vitatenda haki.
Kadhalika alisema jambo lingine lililoishtua familia yake ni pale vyombo vya habari vilivyoeleza kuwa wazazi wa binti huyo ni wahadhiri wa chuo hicho ambacho watoto hao wanasoma jambo ambalo si la kweli.

Taarifa kutoka kwa Kamishna wa Polisi Jimbo la El –Wak Kenya, Nelson Marwa zinaonesha kuwa wasichana hao watatu walikuwa wanakwenda Somalia kupata mafunzo ya kigaidi na baadaye kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga.
Kutokana na kuwepo taarifa kwamba msichana huyo alikuwa anakwenda kuolewa na Askari wa Kikundi hicho cha kigaidi, Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba alisema kama alikwenda kuolewa haina haja ya kukamatwa kwani suala la ndoa lipo kijamii.
Hata hivyo, mpaka sasa wasichana hao bado hawajafunguliwa mashtaka yoyote japo mahakama ya nchini humo imeliruhusu jeshi la polisi kuwashikilia kwa siku 20 kwa ajili ya upelelezi.
-NIPASHE
Note: Only a member of this blog may post a comment.