Wednesday, April 29, 2015

Anonymous

PICHAZ: MITEGO YA WADADA YAMPA WAKATI MGUMU MAFUFU WA BONGO MUVI!

Gladness Mallya
MSANII wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu ametoa kali ya mwaka kuwa mashabiki wake wengi wa kike, wanamtaka kimapenzi licha ya ukweli kwamba katika kazi zake nyingi, anacheza sehemu za kutisha.
Msanii wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu akiwa katika pozi na warembo.
Msanii huyo alitoa kauli hiyo hivi karibuni baada ya kunaswa na paparazi wetu akiwa amezungukwa na warembo huku akiwa amempakata mmoja wao katika sherehe moja iliyofanyika ndani ya Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar. 

“Hapa nimemkataza mke wangu asije kwenye hii sherehe maana angetibuka tu, wanawake wengi mashabiki wangu wananitaka kimapenzi kama hivi unavyoona wananizunguka na kunibusu, sijui wananipendea nini maana mimi filamu zangu nacheza sehemu zile za kutishatisha,” alisema msanii huyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.