Tuesday, April 14, 2015

Anonymous

Mengine yaliyoripotiwa Kenya baada ya kutokea shambulio Chuo Kikuu Garissa Kenya..

Familia za wanafunzi 142 kati ya  148 waliouawa katika shambulio la kigaidi la Al Shabaab kwenye Chuo cha Garissa Kenya wameruhusiwa kuchukua miili ya ndugu zao kwa ajili ya mazishi ambapo Serikali ililazimika kutumia mashine maalum kutambua miili ya baadhi ya watu ambayo iliharibika vibaya kutokana na majeraha ya risasi.

Hilo limeendelea lakini bado kuna ishu oinawaacha watu njia panda,  zaidi ya wanafunzi 166 hawajulikani walipo, familia zao bado zimeendelea kulalamika kutokana na baadhi ya ndugu zao kutoonekana. 

Uamuzi mwiingine mgumu uliotangazwa na Kenya ni kulitaka Shirika la Wakimbizi UNHCR ndani ya miezi mitatu kufunga kambi ya wakimbizi  iliyoko mashariki mwa nchini hiyo, pamoja na kuwarudisha kwao wakimbizi ambao ni raia wa Somalia zaidi ya laki nne. 
Bonyeza play kusikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24
#RIP kwa ndugu zetu waliofariki kwenye shambulio hilo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.