Saturday, April 18, 2015

Anonymous

MBOMBO NGAFU! Simba SC, Mbeya City zatikisa jiji!

Musa Mateja, Mbeya
HABARI ya Mbeya kwa sasa ni mechi ya Ligi Kuu Bara inayochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine kwa kuzikutanisha Mbeya City na Simba.
Tayari mashabiki wengi wameonekana kuwa na pilikapilika za mchezo huo huku kukiwa na kumbukumbu ya Simba kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Wakati Simba ikipambana kujihakikishia kufika nafasi ya pili ikiwa na pointi 35 katika nafasi ya tatu, Mbeya City inapambana kuhakikisha haiingii katika hatari ya kushuka daraja kwani ipo nafasi ya kumi ikiwa na pointi 25. 

Kocha wa Simba, Mserbia, Goran Koponuvic, akizungumzia mchezo huo, alisema: “Huu ni mchezo mgumu kwangu, tunatakiwa kupambana sana ili tupate ushindi, japokuwa hatutakuwa na Okwi (Emmanuel) kwani mwanzo walitufunga hawa jamaa.” 

Kwa upande wa Mbeya City, ofisa habari wa timu hiyo, Dismas Ten, alisema kikosi chao kimeandaliwa vizuri na hakina hofu yoyote dhidi ya Simba.
“Simba ni timu ya kawaida sana na tumejiandaa kama tunavyojiandaa kucheza na timu nyingine za ligi kuu, tunahitaji pointi tatu na wachezaji wote wako fiti kwa ajili ya mchezo huu,” alisema Ten. 

Wakati huohuo jana Ijumaa Stand United walitoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, huku leo Azam wakicheza na Kagera Sugar na kesho Jumapili Mtibwa Sugar watacheza na Prisons huku Ruvu Shooting wakiumana na JKT Mgambo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.