Tuesday, April 7, 2015

Anonymous

Mbinu za Magaidi, Gwajima Aponywa na Maaskofu wa Japan, mashine za BVR zawasili na radi yaua watano Geita…#PBCloudsFM

01TC30-IM1002-zanzibar-island-1475
POWERBREAKFAST ya Clouds FM imefanya uchambuzi wa story kubwa zote za kwenye kurasa za Magazeti Tz, kama ulikuwa mbali na Redio yako basi unaweza kusoma na kusikiliza stori zote zilizosikika hewani leo April 07, hapa. 

April 07, ni sikukuu ya KARUME DAY ikiwa ni  kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza Zanzibar, Abeid Amani Karume, Mwenyekiti wa jumuia ya wafanyabiashara amesema hakuna dalili za viongozi waliopo madarakani kumaliza mgogoro uliopo kati ya wafanyabiashara na TRA, Mkurugenzi wa taasisi ya Mw. Nyerere, Joseph Butiku amesema mambo ya msingi yaliyotolewa kwenye Katiba mpya yarejeshwe, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa amesema haelewi ni kwa nini Serikali imeshindwa kuteketeza meno ya Tembo na wagonjwa wanaolazwa katika Hoptitali ya Wilaya ya Kondoa wanalazimishwa kufanya usafi wodini. 

Magaidi watumia mbinu ya kuwapa mafunzo wananchi wa nchi husika ili kurahisisha kupanua mtandao wao, mashine 248, za BVR zimewasili nchini kwa ajili ya zoezi la kuandikisha wapiga kura, Maaskofu wa Japani wamponya Askofu Gwajima kwa maombi maalumu, wananchi wafanya uharibifu katika treni mpya ya kisasa ya Delux, watu watano wamefariki baada ya kupigwa na radi wakiwa Kanisani huko Geita, waumini wa Kanisa Katoliki jimbo la Mpanda walishindwa kusali baada ya kutokea ugomvi wa kwaya mbili za Kanisa hilo.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza story zote…
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.