Wednesday, April 29, 2015

Anonymous

MASKINI SHETTA! NDOA YAKE HALI YAZIDI KUWA TETE!

Gladness Mallya
KATIKA kuhakikisha anainusuru ndoa yake iliyotikisika kufuatia madai ya kutoka na muigizaji Rose Ndauka, msanii wa Bongo Fleva Nurdin Bilal ‘Shetta’ amemnunulia mkewe gari aina ya Toyota Mark X lenye thamani ya shilingi milioni 19, lakini bibie huyo amelikataa na kuendelea kuishi mbali naye.
Endelea zaidi...
Mke wa Sheta(Leila Yusuf)
Akipiga stori na gazeti hili, Shetta alisema mpaka sasa mkewe huyo, Leila Yusuf bado hajarudi nyumbani kwake kwani alifanya hivyo kama mojawapo ya njia za kuomba msamaha ili mambo hayo yaishe, lakini bado imekuwa ngumu. 

“Nilikuwa sitaki kuzungumzia tena hili suala maana menejimenti yangu ilinikataza, lakini ndiyo hivyo mke wangu bado hajarudi nyumbani na bado tuko kwenye mazungumzo, hata sielewi itakuwaje, nilimnunulia gari ili anisamehe lakini amelikataa, lipo tu nyumbani hapa,” alisema Shetta anayetamba na ngoma yake ya Shikorobo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.