Friday, April 17, 2015

Anonymous

MASKINI MATUMLA! Licha ya Kumchapa Mchina, Hii Ndio Taarifa Rasmi Kuhusu Safari ya Marekani!

Ibrahim Mussa,Dar es Salaam 
WAKATI bondia wa ngumi za kulipwa Mtanzania, Mohammed Matumla akishindwa kupata majibu ya kama atakwenda kuzichapa nchini Marekani au la, taarifa rasmi zinaonyesha nafasi hiyo amepewa bondia kutoka Morocco, Said El Harrack. 

Licha ya ushindi dhidi ya Mchina, Wang Xin Hua, lakini promota aliyesimamia pambano la Matumla na Mchina, Jay Msangi, amesema safari ya Matumla imeshindikana kwa kuwa ameshindwa kufikia vigezo vilivyowekwa na waandaji wa pambano la Manny Pacquiao dhidi ya Floyd Mayweather. 

“Suala la Matumla kwenda Marekani ilikuwa ni moja ya ahadi zetu iwapo atashinda na tulituma mkanda wa video kwa meneja wa Pacquiao ambaye ndiye ameupeleka kwa waandaaji ambao wao wanaamini kwamba Matumla hawezi kupigana siku hiyo kwa kuwa hakufikia vigezo wanavyotaka wao. 

“Matumla alishindwa katika mapambano yake mawili ya nyuma, pia katika pambano dhidi ya Mchina alicheza faulo nyingi, sasa wao wameona ni vema nafasi hiyo apewe huyo Mmorocco,” alisema Msangi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.