Tuesday, April 14, 2015

Anonymous

Majina ya waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Albino yamefika kwa Rais JK?..Mazishi ya waliofariki kwenye ajali.. #PB April14

jazz-radio
Zilizopewa Headlines  kwenye Magazeti leo April 14…
Miili 19 ya watu walioteketea kwa moto katika ajali ya basi na lori Morogoro, imezikwa katika kaburi la pamoja Kilosa, Wasomi na wanasiasa wamesema nchi inapita katika kipindi kigumu kwa sasa kulingana na matukio mbalimbali yanayotokea, Serikali imeshindwa kuweka wazi kufungwa kwa shule zake za sekondari kutokana na ukosefu wa chakula, ndoa ya mwanamke mwenye miaka 54 na kijana wa miaka 25 yakwama Dar, Rais Kikwete amesema bado hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif jana alifika mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi ya wafuasi wa chama cha CUF, Serikali imetangaza rasmi ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu Dar na meli ya Mv Liemba kuwa sehemu ya urithi wa taifa, Jeshi la Polisi Katavi linamshikilia mganga wa jadi kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la kichwa cha binadamu na BAWATA imepiga marufuku baadhi ya waganga wanaotoa huduma kwenye nyumba za wageni.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza stori zote…
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.