ITV lifika katika kijiji cha Park Nyigoti wilayani Serengeti na kushuhudia zoezi la kufukua kaburi likiendelea ambapo inadaiwa kuwa marehemu Celina alifariki dunia tarehe mbili ya machi na kuzikwa tarehe tatu lakini tarehe ishirini na mbili ndugu walikuta sehemu ndogo ya kaburi likiwa limefukuliwa ndipo wakataka kuhakiki kuwa mwili wa ndungu yao upo au umechukuliwa. baada ya kupata kibali cha mahakama wamefukua na kukuta viungo hivyo vikiwa vimekatwa na watu wasiyo julikana.
Akielezea namna tukio ilo lilivyo tokea mama wa marehemu Celina Bi Nyahende Kwihamba amesema tukio hilo limewaweka katika mashaka makubwa kutokana na kijiji hicho kushamiri kwa tabia ya ushirikina na kuiomba serikali isaidie kumaliza tabia hiyo.
Kijiji cha Park Nyigiti mara kwa mara kimekuwa na matukio ya kikatili kwani tarehe mbili ya mwezi marchi watu watano waliuawa na wananchim kwa kuwatuhumu kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina na tarehe saba ya mwezi wa pili kijiji jirani cha lubanda waliuawa watu wawili na kuchoma moto nyuma saba kwa kama tuhuma hizo hizo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.