Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walisema wamekuwa na mgogoro na katekista huyo kwa fedha za michango ya wapiga picha wanazotozwa waingiapo kanisani kupiga picha za matukio kama ya sakramenti kusema fedha hizo zinakwenda kufanya kazi gani!
Mwenyekiti wa umoja wa wapigapicha Wilaya ya Kahama, ‘Uwapika’, ’Charles Richard Shinwa akizungumza na paparazi wetu jimboni hapo alisema:
“Tunabaguliwa, kwani tunapoingia kupiga picha kanisani, baadhi yetu tunatozwa sh. 5,000 kwa kila mpigapicha za kawaida mmoja, mchukua video ni sh. 10,000 mpaka 12,000 na baisikeli ukiingia nayo ni sh.700, pikipiki 1,500.”
Shinwa alisisitiza kitendo cha katekista kufanya ubaguzi kwa baadhi ya wapigapicha ambapo wapo wanaotozwa na wasiotozwa si vizuri.“Tumewekewa mistari miwili ya waaumini kupita ili wapigwe picha. Inatuchanganya wakati wa kupiga picha maana mhusika anakuwa upande mwingine na sisi wapiga picha tupo upande mwingine huku tukiwa tumeshalipishwa fedha na kupewa vitambulisho ambavyo havina mihuri na mwisho wa shughuli tunawarudishia,” alisema Shinwa.
Paparazi wetu alimtafuta katekista huyo kutoa ufafanuzi wa tozo za wapigapicha na waumini wanaopiga picha kanisani hapo ambapo alisema:“Fedha zinazotozwa ni za kusaidia wanaofanya usafi wa ndani na nje ya kanisa licha ya kutotangaza ila ni utaratibu wa kwetu sisi viongozi tulioweka kuanzia 2012-2013. Hatukuwashirikisha mapadri, baba paroko na Askofu Roderick Minje.”
Naye Baba Paroko wa Jimbo la Katoliki Kahama, Robert Lujura alipotafutwa alisema:
“Sina taarifa ya aina hiyo, nitafanya kikao na katibu wa jimbo na katekista huyo kwa maelezo ya ufasaha kwa jambo hilo.
“Kanisa hili lina waumini na wapigapicha waingiao kanisani, kama kuna tozo bila kuwatangazia waumini na wapigapicha kama kutakuwa na utaratibu wa kuwatoza fedha za kuingia kanisani ikiwa na baiskeli na pikipiki si sawa.
“Hili ni jambo ajabu kwa katekista kujifanyia maamuzi yenye muono wa kibinafsi pasipo kufuata Neno la Mungu na utaratibu wa kanisa,” alisema baba paroko.


Note: Only a member of this blog may post a comment.