Friday, April 17, 2015

Anonymous

Kingine kuhusu watuhumiwa 10 wa Milipuko Morogoro, vigogo TRL na Ngeleja na kashfa ya Escrow…@PB Clouds FM

Stori kubwa zilizosikika kwenye Magazeti ya leo April 17, kupitia show ya Power Breakfast ya Clouds FM, mchambuzi ni Paul James karibu mtu wangu… 

Dereva aliyebeba watu wanaodaiwa kuwa magaidi huko Kidatu asimulia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Magesa Mulongo amesema taarifa za magaidi kuvamia mkoa huo sio za kweli, Mtanzania abuni kifaa cha kufundishia bila mwalimu, Mkurugenzi wa TEHAMA, Ally Simba amesema sheria za usalama wa mitandao zilizowasilishwa Bungeni hivi karibuni zimetungwa kukidhi matakwa ya kimataifa, Jeshi la Polisi Dar limeanza kuimarisha usalama katika maeneo hatarishi kwa kufanya doria..


Nyingine ziulizosikika… binti anaedaiwa kubakwa na Emmanuel Mbasha vipimo vimeonyesha hakufanyiwa kitendo hicho,  Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amejikuta kwenye wakati mgumu wakati akizungumza na wananchi wa jimbo lake, Waziri Samuel Sitta amemsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya reli Kapallo Kisamfu na Wanafunzi wa shule ya Tusiime wameendelea kufanya vizuri baada ya shule yao kupewa Tuzo. 

Kulikuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa jukwaa la wahariri Nevile Meena ambae ametoa mawazo yake juu ya Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandaowa mwaka 2015, uliopitishwa na Bunge hivi karibuni.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza uchambuzi wa story zote…

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.