KHAA! NDEGE ILIYOTAKIWA KUPELEKA ASKARI GARISSA ILIKUWA INATUMIWA KIFAMILIA!
Ndanu
Munene Mbithi (aliyevaa njano) ambaye ni mtoto wa Kammanda Rogers
Mbithi, akiwa na rafiki zake kwenye ndege ya Jeshi la Polisi la Kenya.
NDEGE ya jeshi la anga la polisi nchini Kenya ambayo ilikuwa itumike
kupeleka askari kwenye Chuo Kikuu cha Garissa wakati mauaji ya kigaidi
yanaendeshwa dhidi ya wanafunzi, ilikuwa iko Mombasa ikitumiwa kwa mambo
binafsi na kamanda wa jeshi hilo, Rogers Mbithi.
Sehemu ya ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa isafirishe askari wajulikanao kama ‘GSU Recce’
kwenda Garissa siku ya Aprili 7, ambapo ilikuja kuonekana kwenye
mtandao wa Instragram picha ya mmoja wa mabinti wa Mbiti wakiwa kwenye
ngazi za ndege hiyo na maneno yaliyoandikwa: "Mombasa ni raha tu".
Maneno mengine yaliyokwenda sambamba na picha hiyo yalikuwa ni: "Hi
Mombasa...#birthdayweekend".
Mkuu wa jeshi la polisi (IGP), Joseph Boinnet, alikuwa amesema awali
kwamba ndege hiyo haikuwepo ili kupeleka askari huko Garissa na amesema
uchunguzi umeanzishwa ili kufahamu ndege hiyo ilikuwa wapi wakati
magaidi wakiua wanafunzi 147.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
KIMATAIFA
on Tuesday, April 14, 2015
Note: Only a member of this blog may post a comment.