Tuesday, April 14, 2015

Anonymous

Jumamosi hii ndio fainali yenyewe! hapa Akon, hapa wale 13 ! details nyingine ninazo hapa

Akon 1
Post hii ni maalum kukufikishia good news ya kitakachofanyika Jumamosi hii ya April 18 2015 ikiwa ni fainali ya shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika ambalo lilibeba washiriki kutoka nchi 13 ambao wamesimama mbele ya majaji Akon, Devyne Stephens na Lynnsha ambao Jumamosi ndio watashirikiana kumtangaza mshindi. 

Jane Matinde kutoka Airtel anakwambia ishu nzima ya kumtangaza mshindi itaonyeshwa  kupitia chanel ya TRACE URBAN ambayo ni namba 325 kwenye DSTV Jumamosi hii tarehe 18 April 2015. 

Ni shindano ambalo lilihusisha washiriki walioanza kwa kupiga simu kuonyesha uwezo wao na kurekodi moja kwa moja ambapo jamaa wamekuja kufanya hesabu na kukuta simu zilizopigwa ni jumla ya milioni mbili na laki tatu na  kufanya namba ya washiriki wa shindano hili kubwa Afrika kuweza kuzidi mashindano ya Ulaya na Marekani kama vile ya voice na idols. 

Washiriki 13 kutoka nchi za Afrika waliingia katika kinyanganyiro cha kutafuta mshindi tarehe 28 machi 2015 ambapo Jumamosi watazamaji na majaji  watachagua na kutangaza mshindi ambaye atapata dili la kurekodi , kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa mwanamuziki nguli wa Marekani ambapo kwa pamoja ni dili lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500,000/= ambapo ni zaidi ya 920000000 za kibongo. 

Show itaonekana Jumamosi hii saa tatu usiku na kurudiwa Jumapili tarehe 19 kuanzia saa kumi jioni hapohapo TRACE URBAN ikiwa ni show itakayochukua dakika 90.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.