Muhali gani mabibi na mabwana, ambao kwa kawaida ndiyo wadau wakubwa
wa safu hii ya kiutu uzima.Baadhi yetu hawataki kukubali, lakini ukweli
ulio wazi ni kuwa mapenzi ndiyo yanaendesha dunia, kwani hata Mfalme wa
Bongo Fleva, Ali Kiba ana kibao chake kinachoukubali ukweli huu kwamba
mapenzi yana-run dunia.
Tukirudi kwenye mada yetu kama inavyojieleza kwenye kichwa cha habari, katika baadhi ya mahusiano ya kimapenzi, wapo wanaochokana haraka kiasi cha kumshangaza mmoja wa wahusika, awe mwanaume au mwanamke, ingawa uzoefu unaonyesha akina baba wengi ndiyo wenye tabia ya kukinai mapema.
Wanaanza kwa kasi na nguvu kubwa, wakipiga simu kila baada ya muda mfupi na sms kila dakika, lakini wakishafanikiwa kukutana kimwili na mwenzake mara moja au mbili, taratibu ukaribu unaanza kuota mbawa, mithili ya mapenzi ya miaka sita au saba iliyopita.
Hali hii inakuwa zaidi kwa wanaume, kwani ikishatokea wamekutana na mwenza wake zaidi ya mara moja, wanaanza kupoteza spidi ya mwanzo, huku baadhi yao wakileta dharau na sababu zisizo maana katika kuhalalisha tabia yao mpya.
Hivi karibuni mwanamke mmoja msomaji wa safu hii, alinilalamikia juu ya tabia ya mpenzi wake aliyekuwa akimsumbua sana mwanzoni, lakini sasa mwanaume amebadilika kabisa baada ya kukutana naye mara tatu faragha.
Nilijitahidi kumpatia ushauri ambao naamini utamsaidia, lakini hapo hapo nikapata wazo la kuandika mada hii hapa nikiamini itawasaidia wengi pia kwa kuzingatia hali hii wanakutana nayo wanawake wengi. Zifuatazo zaweza kuwa sababu zinazochangia hali ya mwanaume kupotea haraka mara baada ya kufanikiwa kukutana kimwili na mwenza wake.
HANA MAPENZI YA DHATI
Kuwa makini, siyo kila anayetamka neno I love you anamaanisha. Wengi wanatawaliwa na tamaa ya kingono tu na hawana mapenzi ya dhati. Na wengi wa wanaume wapya unaokutana nao, wana wapenzi wao tayari.
Ndiyo maana wanaume wengi wa aina hii, wanakimbilia kutaka kukutana kimwili na ili wafanikiwe katika hilo, watatumia kila aina ya mbinu wanazozijua. Unapokutana na wa aina hii, jipange, usije kutafuta wa kumlaumu. Kwa ujumla, akina kaka wa aina hii ni wenye kuongozwa na uchu wa kimwili.
UJUZI FARAGHA
Sayansi na teknolojia zimeleta mambo mengi. Siku hizi watu wanaangalia mitindo ya mapenzi mitandaoni. Wanatamani kukutana na wanachokiona kutoka kwa wapenzi wao. Hivyo wanapokosa, nao hupoteza hamu. Itaendelea wiki ijayo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.