POLISI katika Jimbo la Enugu, Nigeria, wanachunguza vifo ambapo
wanaume wawili wasiokuwa ndugu, waliwaua baba na mama zao katika matukio
mawili tofauti.
Mauaji hayo yalitokea Aprili 26 Jumapili iliyopita na Aprili 27
Jumatatu ya wiki hii sehemu tofauti ambapo muuaji wa kwanza, Chijioke
Onyeke, alimkata baba yake kwa panga mnamo saa 12 jioni katika ugomvi
usiofahamika chanzo chake katika kijiji cha Umuogboagu kaskazini mwa
nchi hiyo.
Mtu huyo alifia katika hospitali ya St. Mary, kutokana na majereha ambapo mtuhumiwa alikamatwa.
Katika tukio jingine, Chidi Agbo, kutoka kijiji cha Igboeze,
kaskasini mwa nchi hiyo, alimpiga mama yake hadi kumwua ambapo pia
sababu ya kufanya hivyo haijulikani.
Chidi naye yuko mikononi mwa polisi.
NA MTANDAO WA PULSE

Note: Only a member of this blog may post a comment.