Ligi kuu ya Hispania imeendelea tena jioni ya leo – huku Real Madrid na Elbar wakifungua pazia la mechi za leo.
Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameziteka tena
‘headlines’ za vyombo vya habari baada ya leo kuiongoza timu yake kupata
ushindi wa magoli 3-0Ronaldo alifungua akaunti yake ya magoli leo kwa mkwaju wa adhabu
ndogo katika dakika ya 21 ya mchezo huo – goli la leo limemfanya Ronaldo
atimize magoli 38 katika La Liga msimu huu.
Goli hilo lilotokana na mkwaju wa adhabu ndogo ni la kwanza tangu
Ronaldo alipofunga goli dhidi ya Bayern Munich katika nusu fainali ya
Champions League takribani miezi 12 iliyopita.
Magoli mengine ya mchezo huo yalifungwa na Javier Hernandez
Chicharito dakika ya 31 na Jesse akamalizia kazi kwa goli zuri dakika ya
83.
FC Barcelona wanaongoza ligi ya Spain wanacheza na Sevilla usiku huu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.