Ishu
ya ajali za barabarani imechukua nafasi kubwa sana kwenye stori za
kwenye vyombo vya habari TZ.. kwanza ni suala la ajali hizo kuongozana
sana.. kingine ni ishu ya idadi kuwa ya vifo ambavyo vimetokana na ajali
hizo.
Leo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohammed MPINGA yuko kwenye headlines; “Watu
waliofariki kutokana na ajali hizi toka hiyo tarehe 11 mwezii wa tatu
hadi hilo tukio la tarehe 14 takribani mwezi mmoja tu wamefariki watu
103 na kujeruhi watu 38.. katika hao watu 103 wengi ni abiria.. sababu
kubwa ya ajali hizi ni makosa ya kibinadamu ambayo kwa kiasi kikubwa ni
uzembe wa dereva.“
“Mweni
January zimetokea ajali 823, February 641, March ni 32.. ukiangalia
idadi ya watu waliokufa kwa mwezi March ni kubwa ukilinganisha na idadi
ya ajali zilizotokea.“– Kamanda Mpinga.
Tumepoteza ndugu, jamaa, marafiki na watu wetu wengi kwenye hizi ajali.. #RIP kwa wote.

Note: Only a member of this blog may post a comment.