Thursday, April 16, 2015

Anonymous

DUNIA IMEKWISHA: ASHITAKIWA KWA KUMTIA MIMBA BINTIYE

MAHAKAMA moja mjini Bungoma nchini Kenya imemshtaki ofisa mmoja wa wadi ya Bukembe kwa kulala na mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 14 kwa zaidi ya miaka miwili baada ya mkewe kufariki mwaka 2013.

Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya, mwathiriwa ambaye ni mjamzito wa miezi minne amesema kuwa mshukiwa huyo ambaye ni babaake amekuwa akimlazimisha kufanya mapenzi naye kila usiku na kumuonya kwamba angemdhuru iwapo angemwambia mtu yeyote.

''Babaangu pia ameninyima fursa ya kwenda sekondari licha ya mimi  kufanya vyema katika mtihani wa KCPE. Mwaka 2013,nilifanya vyema lakini akanilazimisha kurudia darasa. Mwaka jana nilifanya vizuri zaidi lakini anadhani kwamba iwapo nitajiunga na shule ya bweni, nitamkosesha fursa ya kufanya tendo la ngono name, '' mwathiriwa aliiambia mahakama.
Hakimu mwandamizi, Peter Irer,i alimwachilia mtuhumiwa kwa dhamana ya shilingi 100,000 ama pesa taslimu shilingi 20,000.
CHANZO: BBC SWAHILI

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.