Hit song ya Diamond Platnumz iliyomfungulia milango mingi ya
kimataifa ‘Number 1 Remix’ aliyomshirikisha staa wa Nigeria Davido,
umetajwa kuwania tuzo ya ‘Radio AFRO Australia Song of the Year 2014’.
Wasanii wengine kutoka Afrika wanaowania Tuzo hizo ni pamoja na
Davido ambaye ana nyimbo nne zilizoingia, Bebe Cool ana nyimbo mbili,
P-Square wana nyimbo nne. Wengine ni 2Face, AKA, Cassper Nyovest,
Iyanya.
Tuzo hizi hufanyika kila mwaka na wasikilizaji wa Afro Radio ya
Australia hupiga kura mtandanoni na msanii atakayepata kura nyingi ndiye
anaibuka mshindi.
Ili kumpigia kura Diamond na kumfanya ashinde bonyeza hapa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.