Shirika la kimataifa la uhamiaji IMO na lile la hisani la Save the Children yamesema kati ya manusura 144 na 150 waliwasili katika mji wa Reggio Calabria uliyoko kwenye ncha ya kusini kabisaa mwa Italia Jumanne asubuhi.
Save the Children ilisema katika taarifa ikiwanukuu manusura hao, kwamba kulikuwepo na wahanga 400 wa ajali ya boti hiyo, na kufafanua kuwa miongoni mwa waliookolewa ni pamoja na wavulana na watoto wadogo.

Save the Children ilisema katika taarifa ikiwanukuu manusura hao, kwamba kulikuwepo na wahanga 400 wa ajali ya boti hiyo, na kufafanua kuwa miongoni mwa waliookolewa ni pamoja na wavulana na watoto wadogo.
Msemaji wa IMO nchini Italia Flavio Di Giacomo aliliambia shirika la
habari la Ufaransa AFP, kwamba manusura kadhaa waliliambia shirika lake
kuwa kulikuwepo na watu kati ya 500 na 550 kwenye boti hiyo wakati
ilipozama. Uchunguzi wa awali unaashiria kuwa boti hiyo huenda ilizama
baada ya abiria kuanza kutembea baada ya kuiona timu ya uokozi ya
Italia.
Wakimbizi waliookolewa wakiwasili katika bandari ya Porto Empedocle katika jimbola Sicily siku ya Jumatatu.
Mjadala waibuka upya Italia
Janga hilo la karibuni linakuja wakati maafisa nchini Italia wakisema
karibu wahamiaji 8,500 waliokolewa baharini kati ya Ijumaa na Jumatatu,
na hivyo kuwasha upya mjadala nchini Italia, juu ya iwapo nchi hiyo ina
wajibu wa kuwapokea na kuwahifadhi wahamiaji wote wapya wanaowasili.
Kuboreka kwa hali ya hewa katika bahari ya Mediterrania hivi karibuni
kumesababisha ongezeko la wahamiaji wanaojaribu kuwasili nchini Italia
kwa kutumi boti. Hali inayozidi kuwa ya machafuko nchini Libya, eneo
muhimu wanakoanzia safari wakimbizi, pia imechochea ongezeko la watafuta
hifadhi wanaojaribu kufika barani Ulaya.
Serikali ya Italia inasema zaidi ya wahamiaji 15,000 wamewasili mpaka
sasa katika mwaka huu wa 2015. Wizara ya mambo ya ndani ya Italia
imeziamuru wilaya zote za kanda kutafuta makaazi ya dharura kwa ajili ya
wahamiaji 6 500 -- hatua iliyokosolewa na upinzani, ambao unahoji kuwa
sera ya kuwaokoa wahamiaji inawapa moyo wengine kujaribu safari hiyo
hatari.
Wapinzani Italia watishia kugoma, Ugiriki yajiandaa
Kiongozi wa chama kinachopinga wahamiaji cha Northern League Matteo
Salvini, aliwataka viongozi wa serikali za wilaya kutoka chama chake
kukataa kuwapokea wahamiaji wapya, akiandika kwenye ukurasa wake wa
facebook kuwa chama hicho kiko tayari kuzikalia hoteli, mabweni, shule
na hata kambi zilizoandaliwa kwa ajili ya wimbi jipya la wakimbizi.
Ugiriki ilisema siku ya Jumanne kuwa inapanga kuunda vituo vya mapokezi
bara, kushughulikia wimbi jipya la wahamiaji kutoka visiwani. Uamuzi huo
katika kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na
waziri mkuu Alexis Tsipras, ulifikiwa baada ya wahamiaji na wakimbizi
zaidi ya 700 hasa kutoka Syria na Waafrika kuwaili nchini Ugiriki kati
ya Ijumaa na Jumanne.

Note: Only a member of this blog may post a comment.