Saturday, April 18, 2015

Anonymous

AJALI: Gari La Chama Cha ACT-Wazalendo Lagonga na Kuua Tabora

Moja ya magari yanayotumiwa na chama cha ACT Tanzania baada ya kugonga na kusababisha kifo cha mtu mmoja. 
Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora Susan Kaganda alisema gari hilo lilikuwa linaendesha na mmoja wa madereva anayejulikana kwa jina la Mabona Kabwe lilikuwa likitokea Nzega kwenda Tabora mjini. 

Alipofika eneo la Magiri lilimgonga mwanamke mmoja aliyekuwa akivuka barabara baada ya kushuka kwenye gari alilokuwa amepanda akiwa na mtoto wake wa miezi 10 ambaye aliumia vibaya na kufariki dunia wakati akitibiwa. 
“Gari hilo lilikuwa kwenye mwendo kazi na haikuwa rahisi kuweza kumkwepa mama huyo na kumgonga hapo hapo” Kaganda. 
Hata hivyo mama huyo amehamishwa hospitali ya Kitete kwa matibabu zaidi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.