Majibizano yakendelea.
Hamida Hassan
MSUTO!
Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Sina, mkazi wa Kawe jijini Dar
amejikuta akisutwa mchana kweupe baada kumvujishia taarifa rafiki yake
aitwaye Cheka Komba Mbegere kuwa wanawake wanaojiita Cash Money
wanakwenda kumsuta, Risasi Mchanganyiko lilifuatilia hatua kwa hatua.
Kwa mujibu wa Jamila ambaye naye ni memba wa Cash Money, Cheka alimgombanisha yeye na Sheila kwa kumwaambia kuwa wanatembea na bwana mmoja aitwaye Bubu pasipo kujijua.“Huyu mama amenifanyia kitu mbaya sana, alikuwa anakwenda kumwambia Sheila kuwa mimi natembea na mume wake ambapo tulikuwa tukigombana mara kwa mara na mwisho ndiyo hiyo juzi aliponivamia na kunipiga wakati nimelewa.
“Kwenye ule ugomvi Cheka naye alikuja kunichangia, kesho yake nilipozinduka nilikwenda kituo cha polisi Kawe na kushtaki, asivyo na haya akamuandikia SMS Sheila akimwambia waende kwa mganga ili eti waifute kesi,” alisema Jamila.
Baada ya kuona mambo yameshindakana kwa mganga, Sheila akaona bora amuombe msamaha Jamila ndipo walipomjua ‘mchawi’ wao ni Cheka kisha wakaungana kwenda kumsuta.
“Nilipoona mambo yamenifika shingoni nikaona nirudi kwa mwenzangu nimuombe msamaha tupatane, ndiyo nikamweleza mtu aliyekuwa akituchonganisha tukapanga siku ya kumsuta ambayo ndio leo lakini bahati yake akawa ametonywa akakimbia, tulichunguza tukabaini ametonywa na Sina ndipo naye tukamsuta barabara,” alisema Sheila.
“Hii ndiyo kiboko ya wambeya, kwa aliyeona fedheha hii kamwe hawezi kufanya umbeya wa aina yoyote,” alisikika shuhuda mmoja.
Baada ya kumalizika kwa tukio hilo, paparazi wetu alimvutia waya Cheka ili kumuuliza kama ni kweli alihusika kuwagombanisha Jamila na Sheila na sababu za yeye kutimka nyumbani hapo siku ya tukio.“Mimi nilikimbia kwa sababu walisema eti wamewaita waandishi waje wanisute lakini ukweli ni kwamba mimi sijawahi kuwachonganisha ila walipopigana nilikwenda kuwasuluhisha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.