Kutoka South Africa Rapper A.K.A staa wa hit single ya All eyes on me ft. Burna Boy, Run Jozi na Congratulate ambaye ni miongoni mwa walioalikwa kwenye Zari All White party itakayofanyika Ijumaa hii ya May 1 2015 Dar es salaam amewasili kwenye ardhi ya JK tayari.
Gari la Diamond Platnumz ambalo lina jina la Diamond kwenye plate ndilo lilotumika kumchukua A.K.A mpaka hotelini.
Hii
ni mara yake ya kwanza kwa A.K.A kuja Dar es salaam lakini aliwahi kuja
Zanzibar miaka kadhaa iliyopita ambapo pamoja na kuhudhuria Zari All White Party, stori kutoka kwenye team ya Diamond zinasema mkali huyu ataingia studio kabla ya kuondoka kwa ajili ya kurekodi kolabo yao.
Picha zote kwa hisani ya millardayo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.